Makamu wa Rais ajiandikisha daftari la wapiga kura serikali za mitaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu na kuhakikisha wanajiandikisha.



Akizungumza baada ya kujiandikisha kwenye daftari hilo katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani illiyopo jijini Dodoma, Mama Samia amewataka watanzania kwa ujumla kujitokeza kujiandikindisha ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao na kusisitiza wananchi wanapaswa kuchagua viongozi waadilifu na wenye uzalendo katika kuwatumikia wananchi hasa wanyonge.

"Mimi leo nimeamua kutumia fursa hii kuja kujiandikisha katika mtaa wangu wa Salmini na najua ni haki yangu kuchagua Mwenyekiti wa Mtaa wangu na viongozi wangu kwa sababu najua makazi yangu hapo Dodoma na hawa ndio watakaosimamia mambo yangu kwenye mtaa wangu,”amesema Mama Samia.

”Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha mnapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kuleta maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha

Hivyo amewataka watanzania kuchagua viongozi waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi, wenye maadili ya kuwatumikia watanzania na wenye kutunza rasimali za wananchi wao na ambao watawasaidia viongozi wa ngazi za juu katika kuwatumikia watanzania.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Benelith Mahenge, amesema kuwa  zoezi la uandikishaji ndani ya Mkoa huo limeanza jana na kwamba matarajio yao ni kuandikisha wananchi Laki Tisa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad