Muuguzi Asimamishwa Kazi Akituhumiwa Kubaka Hospitalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BARAZA la Ukunga na Uuguzi Tanzania (TNMC) limeisimamisha kwa miezi mitatu leseni ya muuguzi aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku hadi saa nane msichana mwenye umri wa miaka 16.



Damian Mgaya (41) aliyetoroka anadaiwa kumfanyia hivyo msichana huyo aliyekuwa akimuuguza mama yake katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.



Inaelezwa kuwa mara baada ya kumaliza kumbaka binti huyo aliamua kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi akiwa hajitambui na kummwagia maji mwili mzima.



Inaelezwa kuwa mnamo mwaka 2017, Damiani akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi, aliwahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa polisi na kisha mahakamani na aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018.



Taarifa hiyo imetolewa na msajili wa baraza hilo, Agnes Mtawa, ikisema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka Kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.



Kufuatia mtiririko wa matukio hayo TNMC limeamua kumchukulia hatua ya kusimamisha leseni yake ya kutoa huduma za ukunga na uuguzi popote nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitatu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Afutwe na asiingie tena kwenye taaluma ya utabibu au kufanya kazi ya moja kwa moja na wanawake, watoto na wasiojiweza

    ReplyDelete

Top Post Ad