Nafikiria Kuachana na Yule Mpenzi Wangu Asiyeniomba Hela


Juzi kati hapa nilileta uzi kuwa nimepata mtoto wa chuo na huu ni mwezi wa tatu hajaomba cha vocha wala hela yoyote.

sasa kama mjuavyo vyuo vimefunguliwa wiki hii na hajapata chumba bado nikamshauri akae kwangu kwa sababu ni karibu na chuoni kwao.

so jumatatu akahamia wakati tunashughulikia masuala ya hostel

nilimuacha nyumbani nikaenda kwenye mihangaiko yangu kurudi nyumbani nyumba imepekuliwa kuanzia uvunguni mpaka kwenye dari document zangu zote kasoma japo ziko salama .

wiki mbili zilizopita alipekenyua laptop yangu picha nilizopiga na mademu zangu wa miaka nenda rudi nikamkuta anazicheki.

nikienda choooni anakaa mlango wa choo sijui anasikilizia nini.

nilimkuta ameshika simu yangu na kalamu na karatasi ananakili baadhi ya namba kumuuuliza anachekacheka
sasa huyu ni mpenzi au FBI.

nafikiria kumuacha lakini its too late ananijua kuliko hata mama yangu mzazi maana hadi mikataba ya kazini kwangu juu ya mshahara na kila kitu ninachomiliki anakijua kupitia udukuzi wake
Nishaurini jamani

By mdukuzi via JF

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO