10/09/2019

Nyota Mwingine Aongezwa Katika Kikosi cha Taifa Stars

BEKI wa kati wa Azam FC, Oscar Masai, ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilichoingia kambini jana.

Stars imeingia kambini kujiandaa na mechi mbili, ya kwanza ikiwa ni ya kirafiki na Rwanda 'Amavubi', itakayopigwa  Kigali, Oktoba 14, pamoja na ile ya marudiano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Sudan Oktoba 18.

Masai, ni beki chipukizi, alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana 'Ngorongoro Heroes' kilichotwaa ubingwa wa vijana wa CECAFA wikiendi iliyopita.

Wachezaji wengine wa Azam FC walioitwa kikosi hicho ni Nahodha Msaidizi, Frank Domayo 'Chumvi', Mudathir Yahya, Salum Abubakar 'Sure Boy', Idd Seleman 'Nado' na mshambuliaji Shaaban Chilunda.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger