Ofisi ya Kikwete Yafafanua Hotuba Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


OFISI ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere



Imesema kuwa mada ya Kongamano hilo ilikuwa ‘Urithi wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa’ na  Kikwete alieleza kwa namna alivyomfahamu Mwalimu Nyerere kulingana na mada hiyo



Ofisi hiyo imesema Kikwete ameshangazwa na kusikitishwa kwa kujitokeza watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno yake na kuwepo wanaojaribu kumwekea maneno wakidai eti alikuwa anawasema baadhi ya viongozi waliopo sasa.



Aidha, ofisi imeeleza kuwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na marais waliofuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa pia hakutaja jina la mtu yeyote, hivyo kusikia kuwa  alisema mtu ni jambo linalosikitisha na ni uzandiki, fitna na uchonganishi

Mwisho,  Kikwete amesema alitegemea watu wamkosoe kwa aliyoyasema na si kumsingizia na pia amewataka watu wenye maoni yao wawe wajasiri na kuyasema na si kujificha katika kivuli cha hotuba yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad