Polisi wakabiliana na waandamanaji Barcelona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mamia ya waandamanaji walikabiliana na polisi Ijumaa mjini Barcelona ikiwa ni siku ya tano ya machafuko, tangu waliopohukumiwa viongozi wa wanaotaka kujitenga katika jimbo la Catalonia.

 Waandamanaji hao waliweka vizuizi vya moto na kurusha mawe dhidi ya vikosi vya usalama. Polisi walilazimika kutumia maabomu ya machozi na riasi za mpira ili kuwatawanya.

Kwa mujibu wa gazeti la Uhispania la kila siku la El Pais, watu 17 walikamatwa Ijumaa. Mamlaka za afya zimesema watu 62, walijeruhiwa kutokana na mandamano hayo.

Nayo wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema zaidi ya maafisa wa ulinzi 200 wamejeruhiwa. Maandamano jimboni humo yamesababisha shirikisho la soka la nchi hiyo kuahirisha mechi ya La liga kati ya timu za Real Madrid na Barcelona kutokana na sababu za kiusalama.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad