10/05/2019

Rais Magufuli Amtetea Mkurugenzi Aliyechongewa

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema hatamfukuza kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilejem mkoani Songwe, Haji Mnas kwa kuwa hana taarifa za wizi zinazomhusisha.

 Mbene kusema mkurugenzi huyo hana ushirikiano na viongozi mbalimbali na kusababisha changamoto katika utendaji.

Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene aliyewahi kuwa naibu waziri wa viwanda na biashara alipopewa amesema mkurugenzi huyo amekuwa hatoi ushirikiano kwa wenzake na hatekelezi majukumu yake ipasavyo na kwamba tatizo hilo limekuwa likielezwa kwa viongozi mbalimbali na pia mkoa umelifanyia kazi.

Akijibu tuhuma hizo, Rais Magufuli amesema ‘Kuhusu hili la mkurugenzi unajua kwa watu ambao hawaijui Ileje unaweza ukashangaa, sina uhakika kama dhambi zote hizo ni za mkurugenzi.Taarifa niliyonayo mimi, na (Seleman) Jafo (Waziri wa Tamisemi) ni shahidi kwamba huyu mkurugenzi saa nyingine anaacha kazi zake za ofisini anaenda kufundisha darasani,” Ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia wananchi kwenye mji mdogo wa Mpemba ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Songwe
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger