10/12/2019

Rais Magufuli ataja idadi ya watu walioomba msamaha kwa DPP

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema hadi leo watu 138 wanaodaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi  wameomba msamaha kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo mjini Mpanda wakati akizindua safari za ndege kutoka  Dar es Salaam - Mpanda

“Leo nilikuwa nazungumza na DPP alikuwa ananipa taarifa za wale watu waliotubu na wakaachiwa. Waliokuwa mafisadi wamerudisha fedha, Mpaka leo wamefikia 138, wamesharudisha baadhi ya mabilioni ya fedha, na hao 138 wameshaachiwa wako huru wameenda kujumuika na familia zao na huu ni upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha ” amesema Rais Magufuli.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger