10/06/2019

Rais Magufuli Atoa Siku 5 TANROADS Wahame OfisiRais Magufuli ametoa siku tano kwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuhama katika jengo walilopanga na kuhamia katika jengo la Serikali.

Magufuli ametoa uamuzi huo leo Jumapili, Oktoba 6, 2019 na kumweleza Mtendaji Mkuu wa tanroad Patrick Aron Nipilima Mfugale wakati akizungumza na wananchi wa Sumbawanga wakati wa kuzindua Barabara ya Tunduma – Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 223.1 katika eneo la Laela mkoani Rukwa.

Aidha, Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa Watendaji akiwamo Mkurugenzi na Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kuhamisha makazi yao kutoka Sumbawanga Mjini na kuhamia katika mji mdogo wa Laela ili iwe rahisi kuwahudumia wananchi wa maeneo hayo.

Pia, ametoa mwezi mmoja kwa taasisi nyingine za Serikali zilizopanga kwenye majengo ya watu binafsi kuhamia majengo ya serikali.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger