RC Chalamila atangaza bakora kwa wasioa na kuolewa Mbeya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema anampango wa kuja na bakora ili kuwacharaza wanawake na wanaume mkoani kwake, ambao hawajaoa au kuolewa.

Ameongezea kuwa akishamaliza kuwachapa, atawaagiza waende wakatafute wapenzi wao wa kufunga nao ndoa.

Chalamila ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya, ambapo amesema njia ya kutumia bakora ni miongoni mwa njia ambazo zinasaidia sana kwenye kuhamasisha jambo.

“Siku hizi tunatumia bakora katika kila jambo, tukikukuta umekaa nyumbani na huolewi ni bakora tu nenda katafute mume na ukiwa umekaa nyumbani huoi ni bakora tu nenda katafute mke, kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe” amesema Chalamila.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unaweza ukataka kuoa lakini yule unayetaka kumuoa akawa hayupo tayari kuolewa na huwezi kumlazimisha kama una mpenzi asiyetaka kuolewa. Kama unataka hilo pitisha sheria kali ya kiislamu mtu akikutwa anazini anacharazwa viboko hamsini na guest house zipigwe marufuku maana ni kichaka cha zinaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad