10/05/2019

Samatta Ashusha Pumzi

BAADA ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Napoli ya Italia kwenye uwanja wao wa nyumbani, nahodha wa KRC Genk na Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunguka kuwa kitendo cha kutoka 0-0 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwao ilikuwa ni nafuu kuliko kipigo ambacho walipata awali dhidi ya RB Salzburg.

Genk, juzi Jumatano ilishindwa kutamba kwenye Uwanja wa Luminus baada ya mchezo wa kwanza Hatua ya Makundi kufungwa mabao 6-2 na Salzburg.

“Tumecheza dhidi ya Napoli ambao ni wagumu kweli, lakini tulipambana na hatujapata matokeo mabaya kama ambavyo ilikuwa kwa Salzburg.

“Ilikuwa muhimu kwetu kupata sare kwenye ligi hii, tulipata nafasi hatukutumia vizuri, nao kwao ilikuwa hivyohivyo,” alisema Samatta. Msimamo kamili wa makundi ya Uefa soma ukurasa wa 18.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger