10/06/2019

VIDEO: Waziri Shonza amwomba radhi Magufuli wananchi kumchagua mbunge wa upinzani


Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Juliana Shonza amewaombea radhi wananchi wa jimbo la Momba kwa kuchagua mbunge wa upinzani na kuahidi hilo halitajirudia.

Shonza ameomba msamaha huo mbele ya Rais John Magufuli aliyekuwa njiani kutoka mkoa wa Songwe kwenda Katavi akiahidi kosa hilo halitafanyika tena mwaka 2020 kwa kuwa upinzani hautapewa nafasi.

Mbunge wa Momba ni David Silinde wa Chadema.

“Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa niaba ya wananchi, tunaahidi hatutarudia makosa, upinzani hautakuwa na nafasi katika mkoa wa Songwe kuanzia viongozi wa chini hadi juu kote itakuwa kijani,” amesema Shonza.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amewataka wakazi wa jimbo hilo kuwalaumu viongozi wao kwa kushindwa kutatua kero ya uhaba wa maji.Mwananchi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger