Waziri Mahiga: Kompyuta Zilizoibiwa Si za DPP

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekanusha kuwa hakuna kompyuta za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) zilizoibiwa kama ilivyoripotiwa, bali vimeibiwa vipande viwili vya kompyuta za Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar es Salaam.



Dk. Mahiga amesema nyaraka zote zilizoko kwenye Ofisi ya DPP, Biswalo Mganga,  na taarifa muhimu za wahujumu uchumi hazijaguswa, ziko salama.



“Ofisi ambayo ilivunjwa na vipande vya kompyuta kuchukuliwa ni ya Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu anayeshugulikia Mashitaka ya Serikali haikuguswa, nyaraka zote zipo, taarifa zote zipo na kazi zake zinaendelea,” amesema.



Pia amewataka watu kuliachia jeshi la polisi liendelee na uchunguzi wake unaofanywa kupitia vipande vya komputa vilivyobaki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad