Wolper amwandalia zawadi hii mpenzi wake


Muigizaji na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper, amefunguka kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi ambayo ameamua kuyaficha bila kumuonyesha Mwanaume aliyekuwa naye kwa sasa huku akiwaacha watu midomo wazi.


Alivyodakwa na camera za  EATV & EA Radio Digital, Wolper ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano ila hataki kuonyesha kwa sababu ya ubize wa kazi aliyokuwa nao na hawezi kuwa single.

"Mimi kwa kweli nilishajaribugi sana kuwa single lakini siwezi, sina sababu ya kuwa single nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini nipo bize sana na kazi kwa hiyo hata niliyekuwa naye anajua kama nazingatia sana kazi kuliko mapenzi na tunaelewana ila kuhusu kumpost nitampost siku ya Birthday yake", ameeleza.

Aidha akizungumzia zawadi ambayo amemuandalia Mwanaume wake kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake 'birthday' Jacqueline Wolper amesema,

"Zawadi yangu niliyomuandalia ni uwepo wangu kwake kwa sababu ana bahati ya kuwa na mimi ambaye ni Mwanamke haswa pia zawadi ambayo atayahitaji zaidi kutoka kwangu ni mapenzi ya dhati hivyo vitu vingine vitakuja tu" ameongeza.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Wolper amwandalia zawadi hii mpenzi wake  Wolper amwandalia zawadi hii mpenzi wake Reviewed by Udaku Special on October 09, 2019 Rating: 5

2 comments:

  1. Rajjiiiyyyy..bahati yako.

    Nsiki zawadi kitita milioni nzima.

    ReplyDelete
  2. Tumewazoea wanawake wa kibongo mnapenda sana kujisifu eti nyie ni wazuri, mimi nawaambieni mwanamke mzuri huwa hajisifu yeye hujiona ni wa kawaida ila watu ndiyo hummwagia sifa kemkem, ukiona mtu anajisifia elewa huyo ni mtu mwenye nyodo na dharau na hafai katika jamii.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.