Aika, Nahreel kutangaza tarehe watakayofunga ndoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wapenzi ambao ni wasanii wanaounda kundi la "Navy Kenzo" Aika na Nahreel wamesema hawajahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au bado, ila huwa wanaulizwa zaidi ndoa yao itakuwa lini.

Wakipiga stori na EATV & EA Radio Digital Navy Kenzo, wamesema kwenye mahojiano yao mengi hawajawahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au hawajafunga.

"Nyinyi mtajuaje kama ndoa haipo labda tumeshafunga, halafu hakuna mtu ambaye amewahi kutuuliza hilo swali, watu wanauliza ndoa lini labda kwa sababu hatujaweka mitandaoni ila kwaajili ya Watanzania tutatangaza hivi karibuni tutaweka tarehe na location" wamesema Navy Kenzo.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 10, tangu walipokutana chuoni nchini India, na wamebahatika kupata watoto wawili wa kiume ambao ni Gold na Jamaika.

Aidha kundi hilo la Navy Kenzo wamesema wataachia kazi zao mpya kwa mfumo wa "EP"  ambayo itaanza siku ya Ijumaa ya November 22.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad