Baba Levo Aachiwa Huru, Zitto atoa neno

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini (ACT-wazalendo), Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, leo Novemba 21, 2019, ameshinda Rufaa yake na kuachiwa huru katika Mahakama kuu Mkoa wa Kigoma.

Baba levo alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani, Katika hukumu ya leo, Jaji amefuta hukumu ya mahakama ya wilaya na kumuachia huru.

Awali alihukumiwa kifungo cha miezi 6 katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga Agosti 1, 2019, alipokata rufaa katika mahakama ya Mkoa, akahukumiwa kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 jela, ambapo ameshinda katika Rufaa yake mahakama kuu.

 Kupitia mitandao ya Kijamii ya Kiongozi wa Chama cha ACT- wazalendo na Mbunge wa Kigoma Ujiji, Zitto Kabwe amemkaribisha diwani huyo uraiani na kumtaka aendelee na kazi.

“Nashukuru sana kuwa Diwani wetu  ACT Wazalendo amerudi uraiani. Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imeona adhabu ya kuongeza kifungo mpaka mwaka na siku 2 haikuwa halali,”  amesemaKabwe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad