CHADEMA yapewa onyo na Waziri Lugola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuhusiana na msimamo wake wa kujitoa kwenye zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa madai ya kwamba, anadhani mpango huo huenda ukawa na nia ya kuchafua amani.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza jijini Dodoma, ambapo amesema kama Serikali kupitia Jeshi la Polisi, wamejipanga kuhakikisha zoezi zima la uchaguzi linafanyika kwa amani na usalama.

"Nina taarifa kuwa chama kimoja kimejitoa kwenye Uchaguzi, ni imani yangu chama hicho kinaweza kuwa na mipango ya kuvuruga amani ya nchi hii, nitoe onyo hakutakuwa na nafasi ya chama cha siasa kuratibu mipango ya kuvuruga amani, Serikali tumejipanga kutumia nguvu hakuna amani inavurugwa" amesema Kangi Lugola.

Ikumbukwe hapo jana CHADEMA kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kilitangaza azimio la kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kile walichokidai kuna baadhi ya mambo hayako sawa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad