11/20/2019

Hii Hapa Kauli ya Jose Mourinho baada ya kupewa kazi Tottenham


Mara baada ya kukabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha  Tottenham inayoshiriki Ligi kuu ya Soka ya Uingereza (EPL), kocha Jose Mourinho afunguka.

Ikumbukwe Jose Mourinho amechukua nafasi ya Mauricio Pochettino aliyetimuliwa baada ya miaka mitano ya kuinoa Tottenham ndani ya White Hart Lane.

“Nina furaha ya kujiunga na club hii yenye historia nzuri na mashabiki wenye moyo na timu yao. Ubora wa kikosi na mfumo wa kukuza vipaji wa club hii unanifurahisha sana. Kwenda kufanya kazi na wachezaji ambao wananivutia inapa hamasa zaidi” amesema.

Mourinho ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha wa Man United amepewa mkataba mpaka msimu wa 2022/2023.

Jose Mourinho anaongeza orodha ya timu ambazo amewahi kuzifundisha ambazo ni FC Porto, Inter Milan, Chelsea, Real Madrid, Manchester United na sasa ni Spurs.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger