Idris Sultan amuomba radhi Rais Magufuli “kama ile picha ilikukera”... Aelezea Kesi Yake Ilipofikia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa vichekesho, Idris Sultan, leo Alhamisi Novemba 14, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari, amemuomba msamaha Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kitendo chake cha kujifananisha naye na kuweka picha yake katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram.



Idris amesema yeye ni msanii ana njia nyingi za kufikisha ujumbe na alichokifanya ni ubunifu wake akilenga kumfikishia Magufuli salamu ya siku yake ya kuzaliwa.



Amesema kutokana na rais Magufuli kuwa na shughuli nyingi, alitumia picha aliyojifananisha na rais akiwa sehemu yenye utulivu ili aweze kusherehekea siku yake ya kuzaliwa bila kutingwa na majukumu mengine.



“Pamoja na nia yangu hiyo nzuri kwa bahati mbaya imetafsiriwa ndivyo sivyo na kama binadamu nimeona nimuombe Rais mwenyewe msamaha kwa picha ile kama ilimkwaza,” amesema Idris.



Kuhusu kuhojiwa polisi, amesema jalada lake limepelekwa kwa mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP) kwa ajili ya uchunguzi zaidi baada ya polisi kumaliza upelelezi wao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad