Jamani Nitoke Nnje ya Ndoa..?Nahitaji Ushauri Wenu...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa! 

Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na Mungu wangu!

Nimesali sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je, nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25. Kwakweli sijitambui niko njia panda!

Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2 nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!

Sijielewi nahisi naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,

Nina uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!

Hapa najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani inatosha.

Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndoa zinachangamoto nyingi sana, cha msingi kama walivosema waliotangulia ni Kumuomba Mungu pia kuongea na mchungaji, ila wakati mwingine unahitaji muda mwingi wa faragha ukiwa peke yako kutafakari hayo, ondoka nyumbani kwa muda ukutane na watu tofauti wenye mawazo tofauti waliofanikiwa kwenye ndoa na walioshindwa utajua ni wapi pa kurekebisha. Usiache kazi kwasababu ya ndoa maana inaweza pelekea ndoa ikawa ngumu zaidi maana hutoweza kulisha familia, fikiri kabla ya kutenda na tafakari baada ya kutenda

    ReplyDelete

Top Post Ad