Mbunge Aliyesema Aliyewaponda Wahudumu wa ATCL Aomba Radhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MBUNGE wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima leo Alhamisi, Novemba 14, 2019 ameomba radhi bungeni kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu wahudumu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwa hawana mvuto kwa abiria.




Akitoa kauli hiyo Bungeni wiki iliyopita, Mwilima alisema; “Nataka nitanie kidogo, hizi ndege zetu zinafanya kazi nzuri lakini mle ndani hebu tuangalie wahudumu tunaowaajiri, tuangalie wahudumu ambao hata akigeuka abiria wanasema kweli tuna Air Hostess, sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta Air Hostess mfupi, hana mvuto,” alisema Mwilima.



Akiomba radhi Bungeni leo, Mwilima amesema; “Nilitoa ile kauli lengo lilikuwa ni kuboresha shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuwa ile kauli yangu iliwaboa sana Watanzania hasa wanawake nitumie nafasi hii kuomba radhi Watanzania hasa wanawake wenzangu,” amesema Mwilima.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad