google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mtoto wa Bilionea Atekwa Akitoka Gym Kama Mo | UDAKU SPECIAL

Mtoto wa Bilionea Atekwa Akitoka Gym Kama Mo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WATU wasiojulikana wamemteka Shelton Lalgy, mtoto wa mfanyabiashara mkubwa nchini Msumbiji, Juneide Lalgy.



Tukio hilo limetokea jijini Matola jana Alhamisi, Novemba 28, 2019, asubuhi wakati Shelton akirejea nyumbani kutoka mazoezini (gym). Watekaji walimuingiza ndani ya gari aina ya Toyota Noah lenye rangi nyeupe na kutoweka naye kusikojulikana.







Taarifa ya polisi imesema wanalifanyia uchunguzi tukio hilo ili kupata uhalisia wake.  Tukio hilo limetokea wakati wimbi la utekaji lilikuwa limepungua kwa kiasi kikubwa katika miji ya Maputo na Matola.







Kampuni ya  Transportes Lalgy, iliyoanza shughuli zake mnamo miaka ya 1980 ni moja ya makampuni makubwa ya usafirishaji nchini Msumbiji ambalo hufika katika baadhi ya nchi nyingine za kusini mwa Afrika, likiwa na makao yake makuu jijini Matola, mkoani Maputo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad