Mwanariadha wa Kenya Apokea Tuzo ya Heshima


Mwanariadha wa Kenya anayeshika rikodi ya dunia ya marathon Paul Tergat amepokea Tuzo ya Heshima ya Achilles kwenye Tamasha la Filamu la Kimataifa la Riadha (FICA) katika mji wa San Sebastian nchini Hispania. Bingwa huyo mara tano wa mbio za nyika, Juzi Jumanne alikuwa mgeni wa heshima katika sherehe za FICA.

Tergat ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki amefuata nyayo za Bob Beamon miezi 12 iliyopita aliyepokea tuzo kwa mchango wake kwenye michezo.

Wakati anashiriki riadha mapema miaka ya 1990, Tergat alikuwa bingwa maarufu duniani na kuweza kushinda mbio kadhaa za nyika. Tergat amekabidhiwa kombe na Rais wa Shirikisho la Riadha la Hispania ambaye pia ni Mjumbe wa baraza la IAAF Raul Chapado.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Mwanariadha wa Kenya Apokea Tuzo ya Heshima Mwanariadha wa Kenya Apokea Tuzo ya Heshima Reviewed by Udaku Special on November 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.