Rais JPM: Urafiki wa Misaada Haufai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Novemba 8, 2019 amefungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya  Nje wa Nchi za Afrika na NORDIC uliofanyika akatika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.



Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za NORDIC na Bara la Afrika ulioufunguliwa leo Ijumaa (Novemba 8, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema uhuru wa kisiasa uliozipata Nchi za Bara la Afrika hautakuwa maana iwapo Nchi zake zitaendelea klwa wategemezi wa misaada kutoka Nchi tajiri.



‘Ushirkiano wetu na Nchi za NORDIC kwa miaka mingi umekuwa ni utegemezi wa kiuchumi, umejikita kwenye kutoa na kupokea misaada yaani Donor Recipient Relationship, ushirikiano wa aina hii sio endelevu na hauhitajiki katika mazingira ya sasa.



“Ninashauri tubadilike na kujikita katika diplomasia ya uchumi itakayochochea uzalishaji wa bidhaa na biashara baina ya nchi zetu. Viongozi wa Afrika tunapaswa kutambua kuwa mustakabali wa mataifa yetu upo mikononi mwetu, ni lazima tuondokane na aina hii ya ushirikiano’’ alisema Rais Magufuli.



Rais Magufuli alisema kuwa Bara la Afrika lina mambo mengi mazuri yanayopaswa kuwekewa kipaumbele katika kujikwamua kiuchumi kupitia ushirikiano wake na Nchi za NORDIC ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, hivyo kuliweka katika ajenda muhimu inayopaswa kuwekeza msisitizo.



Aidha Rais Magufuli alisema Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa raslimali na vivutio mbalimbali vya biashara na uwekezaji ukilinganisha na Nchi za NORDIC, lakini hata hivyo Mataifa hayo ya NORDIC yamekuwa yakipiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi ikilinganisha na Nchi za Bara la Afrika.



Akitoa mfano Rais Magufuli alisema katika Nchi tano za NORDIC zenye ukubwa wa kilometa za mraba Milioni 3.5 na mwaka 2018 zilikuwa na Pato la Taifa la Dola Trilioni 1.7 kwa mwaka huku idadi ya wananchi wake ikiwa ni Milioni 27 wakati Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1.2 mwaka 2018 lilikuwa na Pato la taifa lenye thamani ya Dola trilioni 2.334, na kuongeza kuwa Nchi za Bara la Afrika lipo jambo linalopaswa kujifunza.



Aidha Rais Magufuli alisema ni wajibu wa Viongozi wa Bara la Afrika kuweka nguvu ya pamoja katika kusimamia rasilimali na maliasili ilizonazo kwa ajili ya kuleta ustawi wa maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, madini, misitu, mafuta, gesi, nishati na mifugo.



‘Asilimia 30 ya ardhi bora ya kilimo duniani ipo Afrika, na kwa mujibu wa takwimu zilizopo Kati ya Nchi 10 bora zinazoongoza kwa kasi ya ukuaji uchumi duniani, Nchi 5 zinatoka Bara la Afrika, hii ni fursa ambayo haina budi kuitumia Afrika katika kuleta maendeleo kwa ustawi wa wananchi’’ alisema Rais Magufuli.



Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania kwa upande wake imepiga hatua kubwa za maendeleo katika Nchi za Bara la Afrika kwa kuwa imeimarisha sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na kuweka mazingira bora ya uwekezaji.



Aidha aliwataka Viongozi wa NORDIC kutumia fursa zilizopo katika Bara la Afrika kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa viwanda vya malighafi, kwa kuwa bidhaa nyingi za Afrika zimekuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa nje ya Nchi, hivyo wawekezaji hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Bara la Afrika.



Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi alisema kwa miaka mingi sasa Nchi za NORDIC zimekuwa rafiki wa kweli kwa Nchi za Bara Afrika ikiwemo Tanzania ambapo tangu uhuru wa Tanzania Nchi hizo zimekuwa zikisaidia ujenzi wa miradi mbali ya maendeleo nchini.



Kwa mujibu wa Prof. Kabudi alisema katika Mkutano huo, Mawaziri wa Nchi za NORDIC na wale wa Bara la Afrika watapata fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi na masuala ya ulinzi na usalama na kuweka mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi hizo kufikia malengo waliyojiwekea.



‘Suala la Mpango wa Maendeleo Endelevu wa mwaka 2030 pia ni moja ya maeneo yatakayojadiliwa na Mawaziri wa Nchi hizi, tutaliangalia kwa undani zaidi suala la mabadiliko ya tabia nchi katika namna bora ya kukabiliana na changamoto zake katika Mataifa yetu ya Bara la Afrika’’ alisema Prof. Kabudi.



Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Ine Eriksen Soreide alisema Nchi za NORDIC zitaendelea kushirkiana na Mataifa ya Bara la Afrika katika kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na mipango ya pamoja ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya binadamu ikiwemo ugaidi na magonjwa ya milipuko.



Nchi za NORDIC zitaundwa na Nchi tano za Sweden, Norway, Finland, Iceland na Denmark pamoja ikiwa na ushirikiano wa Nchi 29 za Bara la Afrika.



“Tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, kwa sababu tuna amani, ukuaji mzuri wa uchumi. Kwa kuwa marafiki zetu wa nchi za NORDIC wamepiga hatua kiteknolojia hususani teknolojia za viwanda tushirikiane kujenga viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao yetu kwa manufaa ya pande zetu mbili,” amesema Rais Magufuli.





-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad