11/17/2019

UCHAMBUZI "Ben POL Hakutoa Bikira ya EBITOKE...MLELA Kidume....


Kutokana na mgogoro unaoendelea wa kimapenzi kati ya Wasanii wawili Ebitoke na Yusuph Mlela sisi kama Skendo TV tumebaini mambo makubwa mawili ambayo ni:-

BEN POL-,Kila mtu anajua kuwa mwaka 2017 msanii Ebitoke alionekana kuvutiwa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva Ben Pol. Ebitoke alionyesha nia yake ya dhati kabisa kwani ilikuwa ni kitu cha kawaida sana kukutana na video zake Instagram akilia sana huku akimuomba Ben Pol amkubalie ombi lake la kuwa wapenzi.

Siku kadhaa kupita aliamua kutangaza kuwa na Ebitoke kimapenzi na hiyo ndio ikawa safari ya Ebitoke imeanza na Msanii Ben Pol huku Ebitoke akidai kuwa ni bikra.

Penzi la Ben Pol na Ebitoke liliyeyuka kama barafu tena kwa ghafla na kimya kikatawala mazima huku Ebitoke akidai kuwa Ben Pol licha ya kwamba walikuwa wapenzi ila hakufanikiwa kufungua mlango,hivyo Ebitoke na Ben Pol walipoachana bado Ebitoke alifanikiwa kuwa na bikra yake.

YUSUPH MLELA-,Mwaka huu 2019 baada ya Ebitoke kuachana na Ben Pol tulishuhudia kuwaona wawili hawa Ebitoke na Mlela wakiwa kwenye dimbwi zito la mapenzi kitu ambacho wengi walidhani ni movie huku wengine wakiwapongeza kwa hatua hiyo na wengine wakimuonya Ebitoke kuwa makini kwani Mlela ni Play Boy.

Mara nyingi Mlela alipoulizwa kuwa Ebitoke wana mahusiano gani kwa ufupi alijibu kuwa Ebitoke ni rafiki angu tu wa kazi kitu ambacho Ebitoke hakukigundua mapema ila alijua pengine ni utani tu ila anapendwa.

Mgogoro wa mapenzi ulianza siku kadhaa zilizopita hii ni baada ya Yusuph Mlela kuonekana na Mrembo mwingine wakila bata kitu ambacho Ebitoke alichukia na alipojaribu kumpigia simu Mlela hakupokea na baadae akaamua kumblock kabisa.

Tangu hapo Ebitoke amekuwa akiishi maisha ya maumivu makali sana na ni juzi tu tumeona video zake kupitia Instagram akilia kwa uchungu kisa mapenzi.

Kilichotokea leo kama umeona video nzima ni kutokana na kushindwa kujizui hisia za kimapenzi kwa Ebitoke. Kitendo cha Ebitoke kuvamia Mkutano wa Mlela na kumshambulia kwa matusi huku akiwa na kaka yake ni ishara tosha kuwa Ebitoke alikuwa ana mpenda Ebitoke asilimia mia. Kaka yake Ebitoke amesikika kwenye Video akisema kuwa Mlela kumuharibia mdogo wake kitu ambacho ni ishara pia kuwa sio maumivu anayopata Ebitoke tu bali mpaka ndugu zake uenda mpaka Famila nzima wanaumia kwa kitendo alichofanya Mlela.

Jambo muhimu tunalopaswa kujiuliza sisi watu wa pembeni ni kuhusu Ben Pol. Ben Pol ndiye mwanaume wa kwanza kuwa na Ebitoke,mbona kipindi wanatengana hatukuona haya ya leo? au Ben Pol kweli hakufungua mlango wa Ebitoke au uenda mahusiano ya Ebitoke na Ben Pol yalikuwa kibiashara tu ndio maana haikuwa noma.

Kama kweli mahusiano ya Ebitoke yalikuwa real au laa! basi Yusuph Mlela bado ataonekana ni kidume kwa kufanikiwa kufungua Mlango wa Ebitoke ila kwa upande mwingine anaonekana kama mtu katili dhidi ya kuchezea hisia za Ebitoke kitu ambacho ni hatari sana kwani chochote kinaweza kutokea tusipokuwa makini.

Mwisho kama Skendo TV tunapendwa kuwashauri wale wote walio katika mapenzi au wanaotaka kuingia,sio jambo jema kumpa mtu moyo wako kwa muda mfupi kwakuwa umemuona ana sura nzuri,smart,Pesa n.k.

Kwenye safari ya mapenzi chochote kinaweza kutokea hivyo sio kitu rahisi kumtambua uliyenae kwa muda huu ndiye atakaye kuzika kesho,tuwe na nidhamu kwenye mapenzi kwa faida ya watoto wetu.

Umejifunza nini?
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger