11/16/2019

Wawili wajeruhiwa katika jaribio la moto Katavi


Watu wawili wamejeruhiwa katika jaribio la moto lililoandaliwa na meneja wa huduma kwa wateja tawi la NMB mkoa wa katavi wakijaribu kujiokoa.Akizungumza na vyombo vya habari katika tukio hilo Hygrace Mwanjuguja ambaye ni Meneja amesema lengo la kuanda  jaribio hilo nikutaka kuona uharaka wa Jeshi la zimamoto pindi tatizo linapotokea

Mwanjuguja amedai kuwa hawakua na lengo baya la kuandaa jaribio hilo licha ya kusababisha majeruhi lakini hali zao zinaendeleo vizuri na waliojeruhiwa mmoja ni muhudumu wa pale Pamoja na mteja na tayari wamepelekwa Hospitari kwa matibabu zaidi.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Katavi, Islael Kutika amedai kuwa baada ya kupigiwa simu walifika eneo la tukio ndani ya dakika tano na kudhibiti moto ambao haujareta madhara makubwa.

Kutika amesema mpaka sasa hakuna uharifu wowote ambao umetokana na moto huo  tofauti na majeruhi wawili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger