12/14/2019

Aliyepata Msamaha wa Rais Magufuli Adakwa Kwa Wizi wa Ng’ombe


Mkazi wa Mikoroshini Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Mustafa Malimi (23) ambaye ni mmoja ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais John Magufuli Desemba 9 mwaka huu, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba Ng'ombe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi mkoani hapo, Wankyo Nyigesa , ng'ombe aliyeibwa alikutwa amechinjwa na mtuhumiwa huyo. Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea Desemba 11 mwaka huu saa 4:00 asubuhi huko Nero Magorofani wilaya ya Chalinze.

"Mtuhumiwa aliiba ng'ombe mwenye thamani ya Sh milioni 1.2 mali ya Otaigo Elisha (30) mkazi wa Pera Chalinze, alisema.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Wafungwa walioachiwa ni lazima warudi tena kwenye uhalifu kwa sababu wakishaachiwa wengi hujikuta hawajui wafanye nini huku uraiani ili waweze kupata mahitaji yao ya msingi hivyo kuwaachia wafungwa maelfu kwa maelfu bila ya kuangalia wataishije huko uraiani ni hatari sana kwa jamii.

    ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger