12/02/2019

Binti Neema Aliekuwa Akisumbuliwa na Uvimbe Kwenye Mkono Amefariki DuniaNa John Walter-Babati

Binti Neema Joel Gege aliekuwa akisumbuliwa na tatizo la mkono amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Baba mdogo wake Samweli Gege.

Muungwana Blog iliripoti juu ya Ugonjwa uliokuwa ukimsumbua binti huyo ambaye alikuwa akiishi na mama pekee baada ya Baba yake kufariki, ambapo watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu waliguswa na taarifa hiyo na wengine wakimchangia ili apate msaada.

Neema (20)  alipelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) na baadae kuruhusiwa lakini baadaye alizidiwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.

 Neema Joel Gege aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo akiwa amepata nafuu lakini usiku wa kuamkia Desemba 1 hali yake ilibadilika ghafla na hatimaye kupoteza Maisha.

 Neema Joel Gege ( 20 ) alikuwa na ndoto ya kusoma na kuwa Mwanasheria, amefariki dunia akiwa nyumbani kwao huko katika kijiji cha Erri kata ya Kiru wilayani Babati mkoani Manyara.
Mwalimu Isaack Makene wa shule ya Sekondari Kiru alikuwa karibu muda wote akimhudumia marehemu  ambaye mama yake hana uwezo wa kukaa muda mrefu au kusimama kutokana na ajali aliyoipata miaka kadhaa iliyopita.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amen.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger