Bombardier ya Tanzania Yaachiliwa Canada, Kupokelewa Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada imeachiliwa na wananchi wajiandae kuipokea katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama tawala cha CCM leo Alhamisi Desemba 12, 2019 jijini Mwanza, Rais Magufuli amesema, “ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiliwa, wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokea na tutaipokelea hapa Mwanza.”

Novemba 23, 2019, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi alisema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”

Alisema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.

Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya  Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.

Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad