12/08/2019

BREAKING News: Bilionea wa Tanzania Ali Mufuruki Amefariki Dunia


Dar es Salaam. Mfanyabiashara Ali Mufuruki  (60) amefariki dunia leo nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mufuruki ambaye ni mwenyekiti mwanzilishi wa Jukwaa la maofisa watendaji wakuu wa  kampuni (Ceo roundtable) amekutwa na umauti akiwa na familia yake.

Mufuruki ni kati ya matajiri wakubwa 10 wa Tanzania akiwa ni mmiliki wa Kampuni ya Infotech Investment Group Limited na maduka ya Wolworth.

Oktoba 18, 2019 Mufuruki alijiuzulu nafasi yake ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania ili kupata muda zaidi wa kuendelea na biashara zake.

Ali Mufuruki atangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Vodacom Tanzania

Mwenyekiti wa sasa wa Ceort, Sanjay Rughan amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kilichotokea saa tisa alfajiri katika Hospitali ya Morningside
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger