Breaking News: Jengo la Ghorofa Sita la Dondoka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kenya ripoti zianasema kuwa jengo la ghorofa sita limeanguka asubuhi ya leo katika eneo la Embakasi jijini Nairobi, huku watu kadhaa wakihofiwa kunaswa chini ya kifusi cha jengo hilo.

Shughuli za uokoaji zikiendelea, watu kadhaa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Haijabainika ni kwanini jengo hilo liliporomoka na ni watu wangapi wamekwama kwenye jengo hilo.Wenyeji wanadai kuwa huenda ikawa watu wengi wamekwama kwani jengo lenyewe liliporomoka mapema asubuhi na wakati huu shule zikiwa zimefungwa.

Wenyeji wanailaumu Idara ya mipango ya Ujenzi nchini kwa kutohakikisha majengo yaliyojengwa ni salama kutumika.Wanadai kuwa Idara hiyo imezembea katika kukagua usalama wa majengo hasa jijini Nairobi na hivyo kuwaacha watu katika hatari.

Hili si jengo la kwanza kuporomoka, mwezi Septemba mwaka huu jengo la ghorofa moja la shule eno la Dogoretti Nairobi liliporomoka na kuwaua wanafunzi saba huku wengine 64 wakijeruhiwa. Mwaka 2015,Jengo jingine la ghorofa sita liliporomoka eneo la Huruma jijini Nairobi na kugharimu maisha ya watu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad