12/13/2019

Fatma Karume Awatolea UVIVU Chadema...Mmekwenda Kuonyeshwa Vifaa Vitakavyotumika Kukutandikeni"Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amewatolea uvivu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kitendo cha kukubali kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya Uhuru.

Fatma Karime alihoji kuwa wanakwenda kuonyeshwa nguvu ya dola na vifaa vitakavyotumika kuwatandika?

Jana Chadema wameeleza kuwa watashiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika ambapo kitaifa yamepangwa kufanyika mkoani Mwanza kesho.

Fatma Karume baada ya kuona taarifa hiyo aliandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Chadema imemkubali mtumwa wake na kuona wapo pamoja.

Alisema kitendo hicho ni sawa na kukubali kula pilipili yaani mtu anafurahi kula kinachokuumiza.

Aliandika ujumbe huu”CDM mnasuffer from Stockholm syndrome. Poleni sana. Sasa mnakwenda ili muonyeshwe nguvu ya Dola na vifaa vitakavyotumika kukutandikeni? Ama kweli you ate masochists!,”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Wee Futuma. Si uliwahi kuwa wakili zamani kabla ya kukushinda kazi..!! Nasikia umeanzisha duka LA fesheni huko Ungonini. Hivi we WA Wapi?? Karibu nyumbani Tandahimba uone Babu na bibi WA bibi. MAMBO ya fesheni hawayajui Kuna kolosho tu. Tena msimu huu zimezaa mpaka utapenda. Cameliusi alikuwa anakuongelea hv punde. Tuna kumissi na koti jeusi kama zamani.

    ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger