Gereza la Butimba Latii Agizo la Rais Magufuli, Wafungwa Waanza Kuachiwa Huru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli siku ya jana kuwasamehe wafungwa 5,533 katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, wafungwa 79 kati ya hao waliokuwa wamefungwa katika gereza la Butimba Mkoa wa Mwanza wameachiwa leo, Disemba 10, 2019.

Rais Magufuli alitangaza msamaha huo katika maadhimisho hayo, akibainisha kuwa idadi hiyo ni kubwa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote na kutaka walengwa ndio waachiwe.

Katika mkoa wa Mwanza wafungwa watakaopata msamaha huo ni 191.

Leo mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amefika katika gereza la Butimba kwa ajili ya kushuhudia utekelezaji wa agizo la Magufuli huku mkuu wa gereza hilo, Hamza Hamza akitaja idadi ya watakaoachiwa.

"Wafungwa wengine ni wahamiaji haramu ambao wataachiwa huru lakini kwa kufuata taratibu za idara ya uhamiaji,” amesema Hamza.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad