Manchester United Yagoma Kumuuza Pogba, Fellaini Kumfuata Mourinho Spurs na Wengine Sokoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kiungo wa kati wa Ubelgiji na klabu ya Shandong Luneng Marouane Fellaini, 32, amepuuzilia mbali tetesi kuwa huenda akahamia Tottenham kujiunga na mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho. (Eleven Sports via Evening Standard)


Manchester United inaamini kuwa itafanikiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, mwezi ujao na huenda pia wakasaini kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mirror)

Manchester United haitamuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal.com)

Paul PogbaManchester United haina mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba


Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Leeds-mzaliwa wa Norway Erling Braut Haaland, 19, anatafakari kuhusu ofa aliopewa na Borussia Dortmund na RB Leipzig lakini anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United na Juventus kabla ya kuamua hatma yake. (Guardian)

Crystal Palace inataka £80m kumuachilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Chelsea. (Evening Standard)Wilfried ZahaCrystal Palace inataka £80m kumuachilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha

Napoli wanatafakari ofa ya pauni milioni 21 kutoka kwa Arsenal ya kumnunua kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ikiwa Gunners haitamruhusu kiungo huyo wa miaka 23 kuondoka kwa mkopo mwezi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa.(Il Mattino – in Italian)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, amesema kuwa “anaridhika” kuwa Paris St-Germain, licha ya kutaka kuhama klabu hiyo ya Ufaransa mwanzo wa msimu. (AS)

NeymarMshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, amesema kuwa “anaridhika” kuwa Paris St-Germain

Tottenham iko tayari kuanza mazungumzo na kipi wa Argentina Paulo Gazzaniga, 27, kuhusu mkataba mpya. (Football Insider)

Kandarasi ya winga wa Chelsea na Uhispania Pedro Rodriguez, 32, inamalizika mwisho wa msimu huu, hatua ambayo huenda ikampatia nafasi ya kuchezea Barcelona kwa mara nyingine. (Sport)

Chelsea huenda ikamnunua tena winga wa Sassuolo na Ivory Coast Jeremie Boga, 22. (Mail)

Barcelona imetuma maafisa wake Milan kujadili mkataba wa Boga. (Sport)

Rangers imemwambia mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kwamba haitamuachilia mwezi Januari. (Football Insider)

Beki wa England Danny Rose, 29, anasema hataki kujadili hatma yake ya baadae na mkufunzi wa Tottenenham Jose Mourinho na kwamba ataendelea mbele na mpago wa kusitisha mkataba katika klabu hiyo. (Mirror)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad