Mbowe Akemea Vitendo Hivi Ndani ya CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekemea vitendo vya rushwa na kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii katika chaguzi za chama hicho.

Mbowe ametoa kauli hiyo katika mkutano wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha). Katika mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wa baraza hilo.

Uchaguzi ndani ya chama hicho utahitimishwa Disemba 19, 2019 utakapofanyika uchaguzi wa katibu mkuu, naibu katibu wakuu Bara na Zanzibar pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu. Disemba 18, utafanyika uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Bara na Zanzibar.

Tayari Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) na baraza la wazee yamepata viongozi wake.

Katika uchaguzi wa Bawacha, Halima Mdee anagombea peke yake nafasi ya mwenyekiti. Wanaowania umakamu mwenyekiti Bara ni Hawa Mwaifunga,  Aisha Luja, Marceline Stanslaus na Mary Nyagabona, kwa upande wa Zanzibar ni Mariam Salum Msabaha, Sharifa Suleiman na Zeud Mvano Abdulahi.

Katika hotuba yake leo Mbowe amesema, “nimesikia kuna harufu ya rushwa katika uchaguzi huu. Leo unatafuta uongozi ndani Chadema kwa rushwa? Hiki siyo chama nilichokijenga.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa M/Kiti wa Zamani .tunaelewa kuwa ulifanya yako kwa wakati wako.

    Sasa tuachie na sisi kwa wakati wetu.
    Kuna tetesi kuwa unataka kwenda kwa Pole pole,Basi nenda kwa Pole pole sana baada ya kupata m/kiti mpya.

    ReplyDelete

Top Post Ad