12/14/2019

Mfungwa Aliyesamehewa na JPM Aua, Naye Auawa


Mtu mmoja ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John Magufuli, Desemba 9, mwaka huu, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania Bara, amedaiwa kuvamia na kuwachoma visu watu 6 huku mmoja wao akifariki dunia hapo hapo.

Tukio limetokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Mjini Bukoba Mkoani Kagera. Inadaiwa kuwa, baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia hadi kumuua.

Mmoja kati ya waliokuwa naye, amethibitisha kuwa alikuwa mfungwa ambaye naye aliachiwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Magufuli.

Aidha, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, ACP Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Huyo alifanya hivyo ili arudi tena gerezani badala yake ameishia mikononi mwa wananchi wasiotaka ujinga wakampiga hadi kumuua, mimi nafikiri wawe wanachunguzwa afya ya akili kabla ya kuachiliwa huru, wengine wakirudi uraiani huwa waakuwa wabaya zaidi na wakiwa uraiani wanakuwa hawajui wafanye nini ili kupata hela za kujikimu kimaisha.

    ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger