Mwakinyo Amvaa Matumla, Atishia Kuacha Kupigana ...Amtaka Kuomba Radhi Kwa Uchambuzi wake Mbaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Bondia Hassan Mwankinyo amejia juu mchambuzi na mwana masumbwi wa zamani Rashid Matumla kutokana na uchambuzi wake kwenye pambano la Mwakinyo siku kadhaa zilizopita dhdi ya bondia Mfilipino Arnel Tinampay

Mwakinyo amekiambia kipindi cha Sports headquarters cha Efm kuwa hajafurahishwa na namna bondia huyo alivyochambua pambano hilo na kumkejeli kocha wake

“Binafsi nimechukizwa sanaa na kitendo cha bondia mstaafu ambaye alikuwa anapoteza mapambano mfululizo Rashid Matumla amenikwaza sanaa kwa kumkosoa kocha wangu baada ya ushindi wa pambano la juzi ilimpasa afurahi kama mtazania mzalendo” amesema Mwakinyo


Aidha Mwakinyo aliongeza kuwa Matumla hana mafanikio yoyote kwenye mchezo huo hivyo hapaswi kuongea chochote na amemtaka kumomba msamaha kocha wake la si hivyo hatashiriki pambano lolote litakaloa andaliwa na kituo cha Azam TvVIDEO: Pambano la round 10 Mwakinyo vs Tinampay ...

“Haikumpasa kumkosoa kocha wangu yeye mwenyewe hakuwahi kuwa kocha mzuri ndo maaan watoto wake hawajafika popote zaidi ya kuvaa masuari mapana tu kama 2 pac, na natoa wito kuwa sitoshiriki pambano lolote litakalo andaliwa na Azam Tv amabalo litamtukia Matumla kama mchambuzi “ amesema Mwakinyo

Ikumbukwe kuwa Mwakinyo alishinda pambano hilo dhidi ya Arnek Tinampay kwa pointi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enyi ndugu zangu, huyu kijana wetu ameshinda pambano lake na ni fahari kwetu sote kama taifa. Ni wakati wa kushangilia ushindi aliotuletea, badala ya kumshambulia kwa meneno ya kukatisha tamaa. Je angeshindwa pambano hilo kwa points hizohizo je ndo tungemshangilia badala yake? Ni wakati wa kushangilia ushindi na kupongeza. Kama kuna dosari za hapa na pale, basi tumwachie kocha wake aliyemsaidia kufikia hatua hii.

    ReplyDelete

Top Post Ad