12/02/2019

Stormzy Aeleza Alivyoipiga Chini VERSE ya Jay Z Katika Wimbo Wake na Ed Sheeran

Hebu fikiria unampata Jay-Z kwenye Kolabo halafu baadaye unamwambia siitaki verse yako! Hii imetokea kwa rapper wa Uingereza Stormzy ambaye ametuelezea namna ambavyo aliipiga chini verse hiyo ya Jigga.

Stormzy na Ed Sheeran wana Kolabo yao iitwayo "Take Me Back To London" na kumbe tungemsikia Jay-Z, lakini kilichotokea kimeelezwa na Stormzy kwenye mahojiano na The Jonathan Ross Show.

Alianza kwa kusema "Tulikuwa wote watatu Studio, Mimi na Ed Sheeran pamoja na Jay-Z. Kabla ya yote Mimi nilikuwa tayari naipenda 'Take Me Back To London' kwa sababu nilijua tutafanya wawili. Ghafla Ed akasema Jay-Z ataingia kwenye hii ngoma. Kiukweli ilinigonga kichwa kwa sababu ni msanii wangu bora." Alisema Stormzy.

Licha ya kuwa shabiki namba moja wa Hov, Stormzy aliona sio muda sahihi wa mkongwe huyo kufanya ngoma pamoja.
-
"Tulipofika studio tukaanza kuandika wimbo, ghafla Jay alisimamisha muziki na kusema; 'Niambieni kuhusu London, nataka kuandika kitu flani cha kushawishi' - Baada ya mazungumzo ya saa 1, Stormzy alimueleza Jay-Z kwamba
-
"Baada ya Jay kukamilisha verse yako, Uwepo katika huu wimbo umebadilisha kila kitu, lakini wewe ni mtu mwenye akili sana, bize na sidhani kama nitaweza kupata tena nafasi kama hii. Lakini kutoka moyoni mwangu, sifikirii kama huu wimbo ni sahihi kwetu. Sijui kwanini nasema hivi lakini huu sio wimbo."
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger