12/03/2019

Wadau Wamtaka Bondia Mwakinyo Kumwomba Msamaha Bondia Rashid Matumla Baada ya Kuponda Uchambuzi Wake

WADAU mbalimbali wa mchezo wa ngumi wamemtaka bondia, Hassan Mwakinyo, kumwomba radhi bondia mkongwe hapa nchini, Rashid Matumla "Snake Boy" kutokana na kitendo chake cha kumponda kutokana na uchambuzi aliokuwa akiufanya wakati wa pambano lake dhidi ya Mfilipino Arnel Tinampay likiendelea.

Rashid Matumla 'Snake boy' ni nguli wa masumbwi Tz alilalamika sana juu uwezo wa Mwakinyo kiufundi, uvumilivu na mambo mengine ikafika pahala akapandwa na hasira kutokana na approach ya game (Muda mwingi yupo kwenye kamba, kitu kilichomfanya kumpa nafasi Tinampay kumshambulia na kumpunguza nguvu za miguu kwa kumpiga mbavuni).

Kwa tukio kama lile Chid kuzungumzia issue ya kocha wake si dhambi kwa kuwa anaexperience nazo, Hivi kwamba Chid hazijui ngumi zinazotoa points kama sisi wandengeleko?

Mwakinyo alikosa vitu vingi kwanza hanyumbuliki, poor coordination yawezekana katika maandalizi yake alikimbia sana kwenye vilima au kwenye ngazi kutafuta stamina pamoja na pumzi ikamchosha.

Nje ya sababu za gloves but Timing ya Mwakinyo ilikuwa mbaya aliingia akitegemea KO Wakati mwenzie hana muda anacheza tu.

Hassan Mwakinyo anatakiwa achukue hii issue kama changamoto mbele ya safari. Usimpake mtu mafuta kwa mgongo wa chupa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger