Aliyepata Division ONE Afariki Akitokea Kuangalia Matokeo yake Kagera

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kijana Honest Mulokozi Juventusi (15) enzi za uhai wake

Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Kijana Honest Mulokozi Juventusi (15) aliyekuwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rubya Seminari ya Muleba Mkoani Kagera, amefariki Dunia  baada ya kugongwa na Gari la Mizigo akitokea kutazama matokeo yake ya Kidato cha Pili.

Ajali hiyo iliyotokea mnamo Tarehe 09 Januari 2020, eneo la Optima Bunazi Wilayani Missenyi ikihusisha  Gari aina ya Roli (Fuso) yenye namba za usajili T612 BGJ mali ya Kanyomoza, likiendeshwa na Dereva aliyefahamika kwa Jina la Felix France Bayenda (27), ambalo liligonga  Pikipiki aina Bajaji Boxer  yenye namba za usajili T 670 BNF Mali ya Kachecheba Brighton  iliyokuwa ikiendeshwa na Marehemu Honest Mulokozi, wakati akitokea kutazama matokeo yake pamoja na matokeo ya Dada yake.

Shuhuda Wa ajali hiyo wanasema marehemu Honest akiwa anaendesha pikipiki hiyo alijaribu kuwakwepa wanafunzi waliokuwa wakitembea upande wake, hivyo akahamia katikati ya barabara na Kwa bahati mbaya tayari Roli hilo likitokea Nyuma yake licha ya Dereva kujaribu kumkwepa, sehemu ya nyuma ya gari hilo ilimgonga na kumsababishia Kifo.

Michuzi Blog tumefatilia matokeo ya Marehemu Honest na kubaini Ufaulu wa Daraja la Kwanza (Division I.7) akiibuka na ufaulu wa
Civics = A, History = A, Geography = A, Bible Knowledge= B, Kiswahili = A, English= A
Physics= A, Chemistry= A, Biology= A, Basic Mathematics s= A, huku taarifa zikieleza kuwa Dada wa Marehemu nae aliyehitimu kidato cha Nne mwaka Jana kafaulu kwa kupata Daraja la Kwanza pia.

Tayari Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo, na Mwili wa Marehemu umehifadhiwa Chumba cha Maiti katika Hospitali ya Bunazi taratibu za mazishi zikiendelea.

Michuzi Blog inatoa pole kwa familia, Walimu na wanafunzi, Ndugu na Jamaa kwa msiba huo Mzito.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMEN

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad