Breaking NEWS: Mo Dewji Arudisha Majeshi SIMBA, "Mimi ni Simba Damu Tupo Pamoja"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ⁦Simba SC Mohamed Dewji ⁦ amerejea kwenye nafasi ya Uenyekiti baada ya jana kutangaza kujiengua kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye fainali ya MapinduziCup2020 dhidi ya ⁦Mmtibwa.

MO Dewji jana alifikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba, MO alifikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya leo ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.

Leo Mo ameamua kuachana na hasira za maumivu ya kufungwa na kuamua kurudi kwenye nafasi yake ambayo awali alitangaza kujiuzulu nafasi yake na kusema kuwa kilichotokea kwenye akaunti zake jana  kilikuwa ni bahati mbaya na yeye ni simba damu bado wapo pamoja.

“Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu , tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba" - MO DEWJ
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad