1/20/2020

Faiza Amuangukia Sugu "Mimi Nimechoka vita na Kuwa Maadui Nisamehe kwa Nilichokukosea"Msanii wa Filamu na Mjasiriamali, Faiza Ally na mama watoto wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu’ amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake na huyo mzazi mwenzake yalivyokuwa hadi kuachana na kudai kuwa kwa sasa awezi kumuongelea vibaya tena kwakuwa anaamani ndani ya moyo wake.

Faiza ameyasema hayo wakati akifanyiwa interview na Zamaradi na kusema kuwa ameyaongea mengi mabaya ya sugu na hajawahi kujibiwa chochote wala kufanywa chochote na kwasasa ameona hamna umuhimu wa kuendelea kumsema vibaya mzazi mwenzake.

"Nimemsema mengi sana sugu kwa ubaya japokuwa hana ubaya huo najua ana mazuri yake ila najua nimemkosea sana lakini siwezi kumuomba msamaha kwasababu kila kitu kinachanzo na haya yote yametokea kwa aliyotengeneza kwasababu uwezi kumpeleka mtu mahakamani bila kukukosea hapo ndo alinikosea" alisema Faiza.

Aliendelea kusema kuwa mwanzo Sugu alikuwa hamuhudumii mtoto ila kwa sasa anatoa mahitaji ya mtoto wake na amemnunulia simu ili aweze kuwasiliana naye hicho ndo kimemfanya apate amani nakuamua kumuacha kumuongelea vibaya.

"Hii ndo itakuwa interview yangu ya mwisho kumuongelea sitamuongelea tena hata nikiulizwa na rais siwezi kusema chochote kwa sasa anawasiliana na mtoto wake kila simu hicho ndicho nilikuwa nakililia kila siku ninachotaka kumuambia mimi nimechoka vita nimechoka kuwa maadui ila mtoto wangu ananifanya nakukumbuka nisamehe kwa chochote nilichokukosea kwa nilichokijua na nisichokujua moyo wangu una amani na nataka hii amani iliyokuwepo iendelee" alesema Faiza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger