Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Hali ya Jangwani si shwari,barabara Yafungwa Toka Alfajili ya leoHali halisi eneo la jangwani, mamlaka zimefunga rasmi matumizi ya barabara ya Morogoro eneo la magomeni kuelekea katikati ya jiji kufuatia kujaa kwa maji eneo la jangwani.

Kwa hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa karibu maeneo yote ya jiji ambapo njia ya kuelekea Kinondoni Mkwajuni eneo la Magomeni Morocco pia maji yamejaa na msongamano wa magari na watu ni mkubwa pia.

Katika hali nyingine Basi la kampuni ya Tahmeed limekwama katika eneo la jangwani baada ya kujaribu kukatisha wakati wa maji hayo yakiwa tayari yamejaa.

Baadhi ya wananchi wametoa wito kwa kuiomba Serikali kuhakikisha wanaleta mpango maalum wa daraja utakaosaidia kuondoa usumbufu wanaopata kila wakati wa eneo hilo linapojaa maji.

Barabara hiyi imefungwa kuanzia majira ya saa 12 asubuhi ambapo jeshi la Polisi limeweka ulinzi mkali kwa raia kutokatisha eneo hilo.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments