Kigwangala Awapa Pole Wanasimba, Ahoji Bilioni 4 za Mo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba, amehoji juu ya matumizi ya Sh. bilioni 4 alizotumia mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo' kulipa mishahara.



Hiyo imekuja kufuatia mwekezaji huyo kuamua kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, muda mfupi baada ya Simba kufungwa na Mtibwa Sugar katika fainali ya Mapinduzi Cup visiwani Zanzibar jana, Januari 13.

Dkt. Kingwangalla amehoji kuwa hizo bilioni nne ambazo Mo amelipa kama mishahara ndani ya klabu hiyo zimefanyika kwa makubaliano gani na kwa kujiondoa kwake katika nafasi hiyo, mishahara itaendelea kulipwaje?.

"Poleni wanasimba wenzangu, ‘kisukari kimetuvuruga’, hivi kuna mtu anaweza kunisaidia? Hii mishahara ya 4bn iliyolipwa na Mo inalipwa kwa makubaliano gani? Isijekuwa ndiyo katika ile 20bn ya manunuzi ya hisa 50%, ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa, italipwaje? #NguvuMoja''

Baada ya mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup kumalizika kwa Simba kupoteza kwa bao moja mbele ya Mtibwa Sugar, bilionea Mo Dewji akaandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuwa hatoendelea na nafasi yake, atabakia kama mwekezaji na nguvu kubwa ataiwekeza kwenye miundombinu na soka la vijana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad