Mokonda: Asiye na Kitambulisho Cha Taifa Wala Namba Ameendekeza Umbea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema Wananchi wa Mkoa huo ambao hadi jana Januari 19, 2019 walikuwa hawana vitambulisho vya Taifa wala namba waliendekeza zaidi umbea kuliko kufuatilia mambo ya msingi
-
Akiwa katika Tamasha la kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole lililofanyika Mbagala, amesema imekuwa tabia kwa Watanzania wengi kuhangaika na mambo yasiyo na msingi na kusahau vitu vya muhimu vinavyohusu usalama wao na Taifa
-
Amesema “Ninafahamu shughuli hii si mpya, wengi tunapenda kufanya mambo siku ya mwisho tena kwa kusubiri adhabu. Lazima tuwe werevu wa kuyajua mambo bahati mbaya tumehamia kwenye umbea badala ya mambo yanayohusu maisha yetu.”
-
Ameongeza, “Unaposubiri hadi ushurutishwe au utishwe maana yake hujui manufaa ya teknolojia katika maisha yako. Kwa tabia hii ndio maana Rais wetu anapata wakati mgumu kueleweka, tunatumia muda mwingi kufuatilia mambo yasiyotuhusu na sio kulinda usalama wa Taifa lako na maisha yako.”
-
Aidha, Makonda amesema kuwa hakuna muda wa kusajili laini utakaongezwa baada ya leo huku akisema, “Yaani kusajili laini yako hadi tukuitie wanamuziki, hii ni aibu haya mambo yanahusu usalama wako na Taifa. Tatizo lenu mnataka maneno matamu sasa sina muda huo maana sitafuti kura kwako.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad