Ndoa Nyingine ya Fey Yanukia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



BAADA ya kutengana na aliyekuwa mumewe, Holly Star na kuripotiwa kuvishwa pete ya uchumba na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Nirrow, ndoa nyingine inanukia kwa msanii Faidha Omary ‘Sister Fey’.

 

Fey ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na Nirrow.

 

Fey ambaye ni msanii wa muziki na filamu amesema, mashabiki wake wakae mkao wa kusikia habari njema kutoka kwake kwani mwaka huu, Mungu akipenda anatarajia kufunga ndoa takatifu na mchumba’ke huyo.

 

“Kila ninachofanya watu wanaona kama natafuta kiki, lakini ukweli ni kwamba, mwaka huu nimedhamiria kufunga ndoa, ninaolewa na mwanaume ninayempenda, naye ananipenda kwa dhati hivyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa sababu hata hivi ninavyoongea tayari mimi ni mjamzito hivyo kinachosubiriwa hapa ni ndoa tu itimie,” alisema Fey ambaye hakujaliwa mtoto na mumewe wa mwanzo.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad