1/16/2020

Wanafunzi Waliofanya Mtihani Gerezani kwa Tuhuma za Mauaji WatusuaWANAFUNZI sita waliofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne gerezani ambao ni kati ya watuhumiwa 8 wanaoshitakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wenzao katika shule ya sekondari ya Katoro Islamic Seminari iliyoko wilaya ya Bukoba, wamefanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu na kupata ufaulu wa daraja la pili na la tatu.

 

Wanafunzi hao wanaoshitakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Mudi Muswadiko ambaye anadaiwa kuuawa kikatili na washitakiwa hao April 4 mwaka jana wakimtuhumu kujihusisha na mapenzi kinyume na maumbile.

 

“Wawili wamepata Division 3, vijana wanne wamepata Division 2, sisi sote tumepata faraja kubwa na tukawa tunajiuliza, hawa vijana pengine wangekuwa nje wangefanya vizuri sana zaidi” Mkuu wa Gereza.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger