2/21/2020

Chuchu HANS Atoboa Siri Nzito 'Mimba 6 za Ray Ziliharibika"Mwanamama mwigizaji wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans amefunguka kuwa, kabla hajampata mtoto wake, Jaden Vincent na mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mimba sita zilishaharibika.  Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Chuchu alisema hiyo ndiyo sababu iliyomfanya kuamua kuficha mimba ya mtoto wake huyo akihofia nayo ingeharibika.

Chuchu alisema kuwa, siku za nyuma alipitia misukosuko mingi kwenye penzi lake na Ray, kwani watu wengi walikuwa hawapendi jinsi uhusiano wao ulivyo wa amani. Alisema kuwa, kila kukicha watu walikuwa wanaibua mambo mapya ilimradi tu wawagombanishe, lakini Mungu mwema alisimama katikati yao na sasa wana amani.

“Unajua wakati ninaanzisha uhusiano na Ray, watu wengi walikuwa hawapendi. “Huwezi kuamini, nilipigwa vijembe sana, kila kukicha watu walikuwa wanaibua mambo mapya, yote hiyo ni kutaka kutuachanisha tu.
“Nakumbuka walivyokuwa wanasema kwamba Ray hana uwezo wa kuzaa, wakaongea sana, lakini baadaye walipokuja kumuona mtoto wetu wakaumbuka. “Hata hivyo, mimi sikuyajali  yote hayo, lakini kubwa lililoniogopesha ni pale nilipokuwa nikishika tu mimba zinaharibika. Ziliharibika mimba kama sita hivi za Ray, hadi nilipokuja kupata mimba ya Jaden, ikabidi niifiche sana watu wasinione hadi nilipojifungua salama.
SOMA HABARI HIZI KUPITIA APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD > HAPA
“Wale waliokuwa wanamsema Ray vibaya kwamba hawezi kuzaa, waliumbuka kwa sababu mtoto alipotoka akawa amefanana kila kitu na baba yake. “Wakabaki wanashangaa tu na niwaambie kitu, siyo kama Ray alikuwa hana uwezo wa kuzaa! Hapana, alikuwa anatafuta mtu sahihi wa kupata naye mtoto,” alisema Chuchu ambaye ni mama wa watoto watatu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger