Mbosso: Pumzika Martha, Acha Mimi Niwasindikize Wanaopendana Kwenye Siku ya WapendanaoLeo ni siku ya wapendanao ambayo baadhi ya watu wanaitumia siku hiyo kueleza hisia zao za upendo kwa wale wawapendao.


Kwa upande wa muimbaji wa WCB, Mbosso siku hii imekuwa ngumu kidogo, ameandika ujumbe mzito kumuandikia aliyekuwa mpenzi wale Boss Matha.

Mbosso “Dear Martha📝 .., Dunia Leo inasherehekea Sikukuu ya Wapendanao.., Watu wanafuraha sana huku duniani.., Rangi nyekundu na Makopa Mujarabu Yametawala sana Leo .., ila Kwangu ipo Kinyume Sana .., kilichonitawala ni “Sura Yako na Ya Mtoto wetu Ibrahim Mbwana Kilungi.., na nimeambiwa tu za Chini chini Siku hizi anaitwa Joseph .., imani Yangu inanambia huko alipo Yupo Salama hivyo basi usiwe na shaka juu Ya hilo.., Lamwisho nikutoe hofu tu Kuwa sasa nimeacha Kulia Mzee Mwenzangu.. “Najitahidi kuilazimisha Furaha japo Moyoni ninamajonzi ..” na Kibaya zaidi nashindwa Kuanza Maisha Mapya pasi na Upeo wako ..
“Kila siku nakuombea na nitazidi kukuombea Roho Yako iwe Kwenye Pepo ya Firdausi inshaallah 🤲.., …Pumzika Martha, .. acha Mimi Niwasindikize Wapendanao Kwenye Siku Yao ya Wapendanao 😔” Written @yasiningitu


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Mbosso: Pumzika Martha, Acha Mimi Niwasindikize Wanaopendana Kwenye Siku ya Wapendanao Mbosso: Pumzika Martha, Acha Mimi Niwasindikize Wanaopendana Kwenye Siku ya Wapendanao Reviewed by Udaku Special on February 15, 2020 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.