2/14/2020

Mino Raiola Aweka Hatma ya Paul Pogba ndani ya Manchester United katika Mashaka Mapya


Paul Pogba "hatowaza" kurudi Juventus kwani "Italia ni kama nyumbani"- kulingana na wakala wake Mino Raiola.

Pogba - ambaye anaendelea kupona kutoka kwenye jeraha la kifundo cha mguu - amehusishwa sana kujiunga na mabingwa wa Serie A Juve au miamba ya LaLiga Real Madrid, huku kiungo huyo wa United akiripotiwa kukosa furaha ndani ya Manchester.

Raiola ameweka hatma ya Pogba katika mashaka baada ya kutazama mchezo wa Juve (1-1) dhidi ya Milan- kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Coppa Italia Alhamisi.

"Italia ni kama nyumbani kwa Paul. Hana tatizo kurudi Juve lakini tutaona kitakachotokea baada ya fainali za Euro," Raiola aliwaambia waandishi wa habari.

"Paul anataka kucheza katika kiwango bora lakini hawezi kutoroka Manchester United ikiwa wapo katika hali ngumu."

Pogba amecheza michezo nane tu kwenye mashindano yote kwa Man United
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger